Home Uncategorized MBWANA SAMATTA YUPOYUPO ENGLAND

MBWANA SAMATTA YUPOYUPO ENGLAND

MBWANA Samatta anayekipiga ndani ya Aston Villa bado yupoyupo ndani ya Ligi Kuu England msimu wa 2020/21 unaotarajiwa kuanza Septemba 12.

Sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya West Ham United imewaweka sehemu salama kwa kuwa mwanzo ilikuwa Kwenye presha ya kushuka daraja.

Jack Grealish nahodha wa Aston Villa alianza kupachika bao dakika ya 84 likasawazishwa na Andriy Yarmolenko dakika ya 85.

Villa inafikisha jumla ya pointi 35 ikiwa nafasi ya 17 huku West Ham United ikiwa nafasi ya 16 ikiwa na pointi 39 zote zimecheza mechi 38.

Zilizoshuka daraja ni pamoja na Bournemouth iliyo nafasi ya 18 na pointi 34, Watford iliyo nafasi ya 19 na pointi 34 na Norwich City iliyo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 21.

SOMA NA HII  AZAM FC YATHIBITISHA KUACHANA NA CHECHE NA MAGANGA, YAWATAKIA KILA LA KHERI