Home Uncategorized MIKONO YA KIPA RAHIM WA MBAO FC NI MIAMIA, YAWEKA REKODI DAKIKA...

MIKONO YA KIPA RAHIM WA MBAO FC NI MIAMIA, YAWEKA REKODI DAKIKA 360


MIKONO ya Rahim Sheikh, kipa anayekipiga ndani ya Mbao FC inayonolewa na Felix Minziro maarufu kama Baba Isaya imeweka lango lake salama kwa muda wa dakika 360 alizokaa langoni.

Kwa sasa Mbao FC imeanza kurejea kwenye ubora wake licha ya kutojinasua nafasi ya 19 ila imefufua matumaini ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara.

Mechi nne mfululizo alizokaa langoni Mbao FC ilikuwa inasaka pointi 12 imesepa na pointi 10 baada ya kupata sare moja ya bila kufungana na Tanzania Prisons.

Kwa upande wa safu ya ushambuliaji imetupia mabao manne ambapo kinara wao namba moja ni Wazir Jr mwenye mabao 10. 


Hizi hapa mechi zake ndani ya dakika 360:-Tanzania Prisons 0-0 Mbao FC, Mbao FC 1-0 Coastal union, Mbao FC 1-0 Polisi Tanzania na Mbao FC 2-0 Lipuli FC.

SOMA NA HII  GUARDIOLA; HAIKUWA RAHISI KUTWAA TAJI LA CARABAO MBELE YA ASTON VILLA YA SAMATTA