Home Uncategorized MSOLLA: SIJAFIKIRIA KUJIUZULU YANGA

MSOLLA: SIJAFIKIRIA KUJIUZULU YANGA


KUFUATIA mwenendo mbaya wa timu ya Yanga msimu huu kwa kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la FA huku baadhi ya mashabiki wakijitokeza na kutaka mwenyekiti wake, Mshindo Msolla ajiuzulu, mwenyewe ameibuka na kusema hajafikiria kujiuzulu katika klabu hiyo.
Yanga ambayo ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 69 katika mechi 37 za ligi ilizocheza, imejikuta ikitoka nje ya reli kutokana na kushindwa kutwaa ubingwa wa ligi pamoja na FA, hivyo kushindwa kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao.
Kwa sasa Yanga inapambania kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili ikishindana na Azam FC nafasi ambayo hawana uhakika nayo hadi sasa kutokana na mwenendo wa matokeo ya timu yao.

Msolla baada ya kupatiwa tuhuma za baadhi ya mashabiki wakimtaka ajiuzulu huku wengine wakidai tayari ameshajiuzulu, amefunguka kuwa, hafikirii hilo na kudai kuwa anaendelea kuitumikia Yanga.
“Hakuna taarifa kama hiyo, sijajiuzulu nafasi yangu, mimi bado ni mwenyekiti wa Yanga, naendelea kuitumikia klabu yangu kila kitu kinakwenda sawa,” alisikika Msolla.
Kufuatia matokeo mabaya ya Yanga, kumekuwa na mihemko kwa baadhi ya mashabiki wa timu hiyo ambao wanataka mwenyekiti wao ajiondoe klabuni hapo kutokana na kushindwa kuisimamia timu hiyo.

Chanzo:Championi
SOMA NA HII  HIKI HAPA KIKOSI MATATA CHA NYOTA ALIWEKWA KWENYE RADA ZA YANGA