Home Uncategorized MUUAJI WA SIMBA AANZA KAZI LEO RASMI

MUUAJI WA SIMBA AANZA KAZI LEO RASMI


BERNARD Morrison leo ameanza mazoezi na wachezaji wenzake kwenye Uwanja wa wa chuo cha Sheria, Dar es Salaam. 

Morrison alikuwa kwenye mvutano na uongozi wa Yanga kuhusu suala la mkataba wake jambo ambalo lilipelekea awe nje kwa muda.

Yeye alikuwa anasema kuwa ana mkataba wa miezi sita huku Yanga ikieleza kuwa ana mkataba wa miaka miwili.

 Suala hilo lilitinga Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo alihojiwa jana na kutoa maelekezo yake.

Ameingia Kwenye rekodi za wageni waliofunga Kwenye dabi kwani aliwatungua bao 1-0 Simba walipokutana Uwanja wa Taifa, wanatarajiwa kumenyana Julai 12. 

SOMA NA HII  MUANGOLA WA YANGA BALAA LAKE SIO LA MCHEZOMCHEZO