Home Uncategorized MTIBWA SUGAR V SIMBA, NI VITA NDANI YA UWANJA

MTIBWA SUGAR V SIMBA, NI VITA NDANI YA UWANJA




UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa unajipanga kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa  Septemba 12 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri Morogoro.


Simba ilianza safari ya kutetea taji lake kwa mchezo wa ligi dhidi ya Ihefu FC, Uwanja wa Sokoine, ilishinda mabao 2-1. Mabao hayo yalipachikwa na John Bocco na Mzamiru Yassin kwa Simba huku lile la Ihefu likipachikwa na Omary Mponda.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa malengo makubwa ya kikosi hicho ni kuweza kutetea ubingwa ambao waliutwaa msimu wa 2019/20 baada ya kucheza mechi 38 na kujiwekea pointi 88 kibindoni.

Tayari kikosi hicho kimesharejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Mtibwa Sugar wao mchezo wa kwanza uliochezwa Septemba 6 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Gairo walitoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana.

Msimu uliopita walipokutana Uwanja wa Jamhuri, Simba ilishinda mabao 3-0 mbele ya Mtibwa Sugar jambo linaloongeza hasira za kisasi kwa timu hiyo.


Simba ikihitaji kuendeleza rekodi za kuitungua Mtibwa Sugar huku Mtibwa ikiwa na hesabu za kuitungua Simba kwa msimu wa 2020/21.

SOMA NA HII  SIMBA: TUPO FITI KUMENYANA NA POWER DYNAMO