Home Uncategorized MWAKALEBELA: MKAPA ALIKUWA MTU WA MICHEZO

MWAKALEBELA: MKAPA ALIKUWA MTU WA MICHEZO


FREDRICK Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa hayati Benjamin William Mkapa aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu alikuwa ni mtu wa michezo na alikuwa akiishi na jamii kwa ukaribu mkubwa enzi za uhai wake.

Mkapa alitangulia mbele za haki usiku wa kuamkia Julai 24 jijini Dar es Salaam, alidumu kwenye madaraka kwa muda wa miaka 10 kuanzia mwaka 1995 mpaka 2005.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mwakalebela amesema kuwa alikuwa akimtambua Mkapa kwa utendaji wa kazi na ushirikiano na watu wa michezo jambo ambalo lilimfanya apendwe na watu wengi.

“Kuondoka kwa Mkapa kwa familia ya michezo pamoja na jamii nzima kiujumla ni alama kubwa na anaacha somo kwa wengine hasa katika masuala ya uongozi, muhimu kumuombea kheri na kufanya yale mazuri aliyokuwa akiyatenda.

“Alikuwa ni mtu wa michezo aliyependa kusimamia ukweli wakati wote, atakumbukwa na ataendelea kukumbukwa daima, mbali na kujenga Uwanja wa Taifa alikuwa akifuatilia pia masuala yote yanayohusu michezo na furaha yake ilikuwa kuona kila kitu kinakwenda sawa.” amesema.

Mkapa inaelezwa kuwa alikuwa ni shabiki wa Klabu ya Yanga enzi za uhai wake.


SOMA NA HII  WANYARWANDA WAFUNGUKA USAJILI WA KIFAA KIPYA CHA YANGA..!!