Home Uncategorized MWINYI ZAHERA AIPA USHINDI YANGA MBELE YA SIMBA, JULAI 12

MWINYI ZAHERA AIPA USHINDI YANGA MBELE YA SIMBA, JULAI 12


KUELEKEA kwenye mchezo kati ya Simba na Yanga wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho,  Mwinyi Zahera aliyekuwa Kocha wa Yanga amesema kuwa anaiga nafasi Yanga kushinda mchezo huo.

Julai 12, Simba itakuwa kazini kumenyana na Yanga, Uwanja wa Taifa majira ya saa 11:00 jioni na mshindi kwenye mchezo huo atamenyana na mshindi wa nusu fainali ya kwanza itakayowakutanisha Sahare All Stars dhidi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Zahera amesema:”Yanga wana nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo wa nusu fainali kwa sababu kiufundi wamekuwa na hamasa kubwa ya kushinda katika mechi dhidi ya Simba, sasa wanachotaka ni kuendeleza pale walipoishia, japokuwa watu wanasema Simba watashinda ila kwangu mimi
ni tofauti.

“Unajua ukiachana na wachezaji wa Yanga lakini uongozi wa GSM wanajua kuandaa timu vizuri katika mechi na Simba sasa lazima wahakikishe wanapata matokeo kwa kuwa ndiyo njia pekee ya wao kupata nafasi ya kucheza fainali, ikiwezekana ubingwa wa kwenda kimataifa, hivyo naamini Yanga watashinda bila tatizo mchezo huo.

“Simba tayari ni bingwa kwa sasa hana cha kupoteza tofauti na Yanga ambao wanahitaji zaidi ushindi hivyo utakuwa ni mchezo mzuri na wenye ushindani mkubwa,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA YAOMBA MSAMAHA BAADA YA KUCHEZESHWA PIRA GWARIDE DAKIKA 180