Home Uncategorized NAMUNGO YALIPIGIA HESABU KALI KOMBE LA SHIRIKISHO

NAMUNGO YALIPIGIA HESABU KALI KOMBE LA SHIRIKISHO


UONGOZI Namungo umesema kuwa unahitaji kutumia dakika 180 ili kutwaa Kombe la Shirikisho litakalowafanya washiriki mashindano ya kimaifa.
Namungo ilikuwa ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuitungua mabao 2-0 Alliance kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Juni 30 kisha Yanga ilifuata usiku kwa ushindi wa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa.
Itakutana na Sahare All Stars kwenye hatua ya nusu fainali itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Sahare All Stars iliifunga Ndanda FC kwa penalti 4-3 baada ya dakika 90 kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Namungo, Hitimana Thiery amesema kuwa wanahitaji kucheza mechi mbili ambazo ni dakika 180 kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
“Tumeweza kutinga hatua ya nusu fainali ilikuwa ni kazi kubwa ya wachezaji kucheza kwa juhudi na kufanya yale ambayo nimewaelekeza, ushindi wetu ni chachu kwa ajili ya mechi yetu inayokuja na tunahitaji kucheza mechi zote mbili ili tutwae ubingwa,” amesema Thiery.
Azam FC ambao walikuwa ni mabingwa watetezi walitolewa hatua ya robo fainali na Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa kwa kufungwa mabao 2-0.

Hivyo Simba itakutana na Yanga, Julai 12, Uwanja wa Taifa na mshindi wa mechi hiyo atakutana na mshindi wa mechi kati ya Namungo na Sahare kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho.
SOMA NA HII  KWA FEI TOTO, MKUDE ANAOMBA POO