Home Uncategorized KAI HAVERTZ ANUKIA NDANI YA CHELSEA

KAI HAVERTZ ANUKIA NDANI YA CHELSEA


KAI Havertz, nyota wa Bayer Leverkusen anatajwa kuibukia ndani ya Chelsea msimu ujao baada ya makubaliano yaliyofanyika na kiongozi wa masuala ya michezo, Rudi Voller ndani ya klabu hiyo.

Nyota huyo mwenye miaka 21 amehusika kwenye jumla ya mabao 23 ndani ya klabu hiyo akifunga mabao 15 na kutoa pasi nane.

Kiongozi huyo amesema kuwa makubaliano ambayo yamewekwa iwapo yatatimia basi nyota huyo atakipiga ndani ya Chelsea.

Kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja, Bayern Munich ambao ni mabingwa wa Bundesliga walikuwa wanahitaji saini yake ila wameamua kujiweka kando baada ya kuona kwamba kinda huyo anapenda kwenda Chelsea.

“Kwa sasa bado ni mchezaji wetu na tuna mipango naye ila tuna matumaini kwamba anaweza kubaki hapa kwa muda, akihitaji kuondoka hakuna tatizo hatuwezi kumzuia,” amesema.

SOMA NA HII  HILI HAPA JESHI LA SIMBA LILILOTIA TIMU MBEYA,KESHO KULIWASHA DUDE