Home Uncategorized TFF YATOA TAMKO KUHUSU ISHU YA MORRISON KUDAI ALICHEZA MECHI MBILI BILA...

TFF YATOA TAMKO KUHUSU ISHU YA MORRISON KUDAI ALICHEZA MECHI MBILI BILA MKATABA


KAMATI ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) imesema kwamba hakuna mchezaji aliyeruhusiwa kucheza ligi bila ya kuwa na mkataba, hivyo kauli ya Bernard Morrison kuwa alicheza mechi mbili bila mkataba ni uongo.
Kamati ya katiba, sheria na hadhi ya wachezaji ya  TFF imesema kwamba hakuna mchezaji aliyeruhusiwa kucheza ligi kuu bila ya kuwa na mkataba.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Elius Mwanjala, ametoa kauli hiyo akitolea ufafanuzi alichokisema mchezaji Bernard Morrison kuwa aliitumikia Yanga katika michezo miwili bila ya kuwa na mkataba.
Mwanjala amesema kauli ya Bernard Morrison ni ya uongo kwa kuwa utaratibu wa wachezaji wote kucheza Ligi Kuu unafahamika, ni lazima awe na mkataba ili kupata usajili na uhalali wa kucheza ligi kuu.
Kuhusu  masuala ya mkataba wa Morrison, Mwanjala amesema wanasubiri kupokea baadhi ya nyaraka kutoka Yanga ili kufahamu uhalali wa mkataba wa miaka miwili ambao mchezaji anakana kuwa hajausaini.
Hata hivyo kamati hiyo imekiri kuipokea mikataba ya miezi sita na miaka miwili ya mchezaji huyo lakini wanasubiri kikao cha mwisho kuzipitia nyaraka zitakazowasilishwa na Yanga.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amesema wanaendelea kushughulikia malalamiko ya Yanga ambao waliyafikisha  katika kamati yao juu ya moja ya klabu nchini kutumika kumrubuni mchezaji wao Bernard Morrison kiasi cha kuukana mkataba wao.
Vilevile kamati imesema itatoa hukumu ya pamoja dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, ambaye amelalamikiwa kuleta taharuki ndani ya Wekundu wa Msimbazi kwa kutangaza katika vyombo vya habari kuwa wamekamilisha mazungumzo na kiungo wao Clautius Chama, kinyume na utaratibu.
SOMA NA HII  POCHETTINO KURUDI TENA SPURS