Home Uncategorized YANGA YAIVUTIA KASI SIMBA, CHIMBO LAKE LIPO HUKU KWA SASA

YANGA YAIVUTIA KASI SIMBA, CHIMBO LAKE LIPO HUKU KWA SASA


MABINGWA wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara bado wapowapo kwa sasa ndani ya ngome ya Kagera baada ya kuitungua bao 1-0 Uwanja wa Kaitaba.

Kwenye mchezo waliocheza jana, Julai 8, majira ya saa 10:00 jioni Yanga iliweza kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza wa ligi uliochezwa Uwaja wa Uhuru.

Mchezo huo ulikuwa wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Luc Eymael kukaa kwenye benchi la ufundi akipokea mikoba ya Mwinyi Zahera.

Leo chini ya Eymael wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa wanatarajia kuanza safari ya kurejea Dar kesho ili kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuvaana na Simba, Julai 12.

Eymael amesema:”Ushindi wetu dhidi ya Kagera Sugar unatupa nguvu ya kuendelea kujiaandaa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Simba.”

Mchezo wao dhidi ya Simba ni wa hatua ya nusu fainali ambapo mshindi wa mchezo huo atatinga hatua ya fainali na kukutana na mshindi wa mchezo kati ya Sahare All Stars dhidi ya Namungo FC.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR YAANDAA DOZI KAITABA