Home Uncategorized JUMA NYOSSO BADO WAMO NDANI YA UWANJA

JUMA NYOSSO BADO WAMO NDANI YA UWANJA

JUMA Nyosso nah

odha wa Kagera Sugar ni miongoni mwa mabeki ambao wapo Makini ndani ya Uwanja muda wote huku akitoa majukumu kwa vijana wake naye akitimiza pia.

Kagere Sugar iliyo chini ya mzawa Mecky Maxime imecheza jumla ya mechi 29 ipo nafasi ya nane.

Safu ya ulinzi iliyo chini yake akiwa ni beki mkongwe imeruhusu mabao 31 ya kufungwa ndani ya dakika 2,610.

Ina wastani wa kuruhusu bao moja kila baada ya dakika 84.

Safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 36 ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 72.

Timu ambayo imeruhusu mabao mengi kwa msimu huu ni Singida United ambayo ikiwa imecheza mechi 29 imefungwa mabao 49 ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 53.

SOMA NA HII  IBRAHIM AME ATAMBULISHWA SIMBA, ASAINI MIAKA MIWILI