Rutanga ambaye hapo awali alithibitisha kuwa amesajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili ambapo alikuwa akisubiri kutumiwa tiketi ili kuweza kuwasili nchini.
Beki huyo amesema kuwa tayari alishasaini mkataba wa miaka miwili wa kukitumikia kikosi cha Yanga na baada ya hapo viongozi walimwambia atulie mipaka ikifunguliwa atatumiwa tiketi ya ndege jambo ambalo limekuwa tofauti mpaka sasa.
“Nilisaini mkataba na Yanga wa miaka miwili baada ya hapo viongozi wa Yanga waliniambia kuwa nisubiri mipaka ya Rwanda itakapofunguliwa lakini nashangaa hali imekuwa tofauti mpaka sasa.
“Nimekuwa nikiwatumia meseji lakini imekuwa kimya na hawajibu kabisa, hivyo nimekuwa na wasiwasi na dili hili ambalo nilikuwa nina uhakika nalo,” amesema beki huyo.
Dili la Rutanga na Yanga linaweza likaota mbawa kutokana na Yanga kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Polisi Tanzania, Yassin Mustapha.