Home Uncategorized BREAKING:MINZIRO AWAGARAGAZA CIOABA NA AMRI SAID,ASEPA NA TUZO

BREAKING:MINZIRO AWAGARAGAZA CIOABA NA AMRI SAID,ASEPA NA TUZO

Habari za Michezo leo

KOCHA wa Mbao FC ya Mwanza, Fred Felix Minziro amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Julai wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), msimu wa 2019/20.


 Minziro amewashinda Amri Said wa Mbeya City na Aristica Cioaba wa Azam aliokuwa akishindana nao.

 Mwezi Julai, Minziro aliiongoza Mbao kushinda michezo mitano kati ya sita waliyocheza ndani ya mwezi Julai na kupata sare moja.

Msimu wa 2020/21 Mbao FC itashiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa kuwa ilitolewa na Ihefu FC kwenye mchezo wa playoffs kwa faida ya mabao ya ugenini.

Mchezo wa kwanza Ihefu ilishinda mabao 2-0 na mchezo wa pili, Mbao ilishinda mabao 4-2 na kufanya zifungane jumla ya mabao 4-4.

 
SOMA NA HII  VIWANJA SABA VYAPIGWA PINI NA BODI YA LIGI