Home Uncategorized KILICHOWAFANYA YANGA WAKAMPA DILI MSERBIA HIKI HAPA

KILICHOWAFANYA YANGA WAKAMPA DILI MSERBIA HIKI HAPA


ZLATKO Krmpotić kwa sasa ndiye Kocha Mkuu wa Yanga ametua leo mapema akitokea nchini Serbia kuchukua nafasi ya Mbelgiji, Luc Eymael aliyetimuliwa Julai 27.

 

Yanga imemchukua kocha huyo akitokea Polokwane City ya nchini Afrika Kusini huku akiwa amefundisha baadhi ya klabu  kama APR (Rwanda), Zesco United (Zambia) na TP Mazembe (DR Congo).

 

Timu hiyo imemchukua kocha huyo baada ya Mrundi, Cedric Kaze aliyekuwa anafundisha Academy ya Barcelona kupata matatizo ya kifamilia.

 

Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM na Mjumbe wa Kamati ya Mashindano wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema :- “Baada ya dili kufeli, haraka tukahamia kwa Zlatko ambaye yeye alikuwa chaguo letu la pili kati ya makocha hao walioleta CV zao Yanga, hivyo kamati ikachukua maamuzi ya kumpitisha Mserbia huyo kuja kuifundisha Yanga,


“Uzoefu wa Zlatko wa kufundisha timu za Afrika ndiyo umetushawishi sisi viongozi kumpa nafasi ya kuja kuifundisha Yanga, kwani aliwahi kuzifundisha klabu za TP Mazembe, Zesco na Polokwane, kocha huyo tumemuachia nafasi mbili za usajili za wachezaji wa kigeni ambazo kama akihitaji mchezaji wake atakayetaka kufanya naye kazi tumsajili,” amesema Hersi.

 

Amewahi kuwa kocha bora kule DR Congo msimu wa 2016-2017, msimu uliofuata pia akawa kocha bora kwenye Ligi ya Zambia akiwa na Klabu ya Zesco pia akawa kocha bora Afrika. Mwaka 2018 baada ya kutua Botswana kuinoa Jwaneng Galaxy aliibuka pia kocha bora wa msimu.

 

“Msaidizi ni Juma Mwambusi ambaye ni mzawa na ni pendekezo la kocha mpya kwamba alitaka kufanya kazi na mzawa.

 

“Pia, kocha wetu mpya wa makipa ni Niyonkuru (Vladimir) ambaye ni raia wa Burundi yupo tayari nchini kwa kufanya kazi yake hiyo, tumeliboresha benchi letu la ufundi kwa ajili ya kufi kia malengo yetu,” alisema Hersi.

SOMA NA HII  MAXI AWAPA WACHEZAJI WA YANGA KAULI HII YA KISHUJAA KUHUSU KIPIGO CHA SIMBA