Home Uncategorized NONGA ARUDISHA MKWANJA NAMUNGO

NONGA ARUDISHA MKWANJA NAMUNGO

 

PAUL Nonga, nyota mpya wa Gwambina FC inayonolewa na Fulgence Novatus, ilimlazimu arudishe nauli kwa mabosi wa Namungo ambao walikuwa wanahitaji saini yake.

 

Nyota huyo aliyekuwa Lipuli, alikuwa anahitajika kwenda kusaini Namungo kabla ya Gwambina FC kumvutia kasi na kumpa mkataba.

Akizungumza na Spoti Xtra, Nonga alisema kuwa awali alikuwa kwenye mazungumzo na Namungo iliyokuwa na nia ya kupata huduma yake, lakini alibadili maamuzi baada ya Gwambina kumfuata rasmi.

 

“Nilikuwa kwenye hatua za mwisho kujiunga na Namungo ila Gwambina walipoonyesha nia niliwaelewa na nikaenda kusaini, kwa kuwa nilitumiwa nauli na Namungo ilinibidi niwarudishie mkwanja wao,” alisema Nonga

SOMA NA HII  SIMBA YAJIFUA LEO SUMBAWANGA KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO