Home Uncategorized SAMAKIBA LEO HAPATOSHI, MORRISON HATIHATI KUKOSA TIMU KWA MKAPA

SAMAKIBA LEO HAPATOSHI, MORRISON HATIHATI KUKOSA TIMU KWA MKAPA

HAPATOSHI leo katika Uwanja wa Mkapa uliopo jijini Dar wakati vikosi vya Timu Samatta na Timu Alikiba vitakapomenyana katika mchezo wa hisani wa SamaKiba Foundation.

 

Mchezo huo una lengo la kukusanya mapato na kuzisaidia jamii zenye uhitaji ambapo msimu huu wamelenga kusaidia katika masuala ya elimu.


Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa timu hizi kukutana, katika michezo miwili iliyopita Timu Kiba walipoteza yote ambapo mchezo wa kwanza walifungwa 3-1 na wa mwisho walichapwa 6-3.

 

Hata hivyo ukiachana na mchezo huo kivutio kikubwa kimekuwa kwenye vikosi vya wachezaji hao ambapo msimu huu Samatta na Ali Kiba wameongeza wachezaji ambao wamefanya vizuri katika ligi msimu huu ambao msimu uliopita hawakuwepo.

 

Timu Kiba wao leo watakuwa na mastaa kama Bakari Mwamnyeto, Bernard Morrison, David Molinga na Shaibu Ally ‘Ninja’ huku Timu Samatta wao watakuwa na Clatous Chama, Deo Kanda na John Bocco ambao msimu uliopita hawakuwepo.

 

 Ali Kiba amesema kuwa, safari hii hatakubali kufungwa na timu Samatta hata kama atatumia njia zake za kuwahonga waamuzi kama ilivyokuwa awali.

 

“Safari hii tumejipanga kuwafunga timu Samatta, hapo awali walitumia njia za kuwahonga waamuzi ili wapate ushindi ndio maana walifunga magoli ya kuvizia,sasa safari hii tutawafunga mabao mengi,” amesema Kiba.


Jana Morrison licha ya kuwa ni Timu Kiba alihama kambi na kuingia kufanya mazoezi kambi ya Timu Samatta, kuna hatihati leo akakosekana kwenye timu zote mbili.

SOMA NA HII  VPL: MBEYA CITY 0-1SIMBA