Home Uncategorized BREAKING:MORRISON WA YANGA ASAINI SIMBA

BREAKING:MORRISON WA YANGA ASAINI SIMBA

 

BREAKING:BERNARD Morrison kiungo mshambuliaji wa Yanga leo ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba.


Morrison mwenye mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara wakati akikipiga Yanga alikuwa kwenye mvutano mkubwa na mabosi wake kwenye suala la mkataba ambapo mchezaji alisema kuwa ana dili la miezi sita huku uongozi ukisema kuwa amesaini dili la miaka miwili.

Leo Agosti 8, Morrison amevalishwa uzi mwekundu na kuonekana akisaini dili jipya la kujiunga na Simba.

Huu unakuwa usajili wa kwanza kwa Simba kutambulishwa rasmi kwa ajili ya msimu wa 2020/21.

Thamani ya dau lake inatajwa kuwa ni zaidi ya milioni 150 ambayo amepewa ili kujiunga na klabu ya Simba huku akitajwa kupewa dili la miaka miwili.




SOMA NA HII  LIVERPOOL IPO KWENYE HESABU ZA KUPATA SAINI YA MBAPPE