Home Uncategorized SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU SENZO

SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU SENZO

 


BAADA ya Senzo Masingiza aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba kujiuzulu ndani ya klabu hiyo huku ikielezwa kuwa amepata kazi ndani ya Simba uongozi wa Simba umesema kuwa Simba ni klabu kubwa.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Haji Manara ameandika:” kwa hiyo mzunguko wa dunia umesimama siyo? Simba ni huge Club (klabu kubwa) our hope (matumaini yetu) kesho Senzo utakuja kukabidhi ofisi na nyaraka zetu kama utaratibu unavyosema. Kifuatacho.
Sababu kubwa inayotajwa kwa Senzo kubwaga manyanga ni kutokana na suala la usajili wa Bernard Morrison ambaye alitangazwa jana kuibukia ndani ya Simba akitokea Yanga.

Inaelezwa kuwa Morrison hakuwa chaguo la Senzo kusajiliwa kwake kumefanya akasirike na kujiweka pembeni.
SOMA NA HII  WALIOMCHIMBISHA SIMBA MKUDE JONAS HAWA HAPA,MECHI 10 NJE