Home Uncategorized WAKATI HUU WA USAJILI MUHIMU KUZINGATIA RIPOTI YA KOCHA

WAKATI HUU WA USAJILI MUHIMU KUZINGATIA RIPOTI YA KOCHA

 DIRISHA la usajili linaendelea kwa sasa ambapo timu nyingi zinajipanga kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Kuna umuhimu mkubwa kwa kila timu kuanza maandalizi mapema kwani matokeo chanya uwanjani yanatengenezwa na maandalizi ya awali ambayo timu huwa zinafanya.

Muda wa kufanya haya yote ni sasa kwa kuanza na usajili makini pamoja na kambi bora zitakazofanya kila timu kupambana kikamilifu msimu ujao.

Kwa timu zote bila kujali zinashiriki Ligi Kuu Bara ama Ligi Daraja la kwanza ni muhimu kujipanga vema.

Wale ambao wamekuwa wakifanya usajili kwa mapezi yao ama kutumia nafasi zao za uongozi si sawa kwani anayejua uhitaji wa wachezaji ni kocha mwenyewe.

Itapendeza endapo viongozi watafuata ripoti ya kocha kwenye kufanya usajil jambo litakaloepusha lawama na malalamiko kwa benchi la ufundi kwani wao ndio wanahusika kwenye suala la kupanga timu.

Kwa kupitia yale mapungufu ambayo benchi la ufundi limeyaona hapo ndipo kazi inabidi ifanyike na sio kusajili kwa kufuata mkumbo.

Kila mmoja amekuwa ana mamlaka hasa linapofika suala la usajili kulingana na mapenzi ambayo anayo kwa mchezaji ama wengine ni wale ambao wanaona kwamba watapata faida endapo watamsajili mchezaji fulani.

Sasa suala la kutazama faida huwa linakuwa kwa muda tu tofauti na yule ambaye atasajili kwa kufuata mapendekezo ya mwalimu itasaidia kujenga kikosi imara.

Ikumbukwe kuwa wakati timu ikiboronga anayepewa mzigo wa lawama siku zote huwa ni kocha hivyo itakuwa vizuri endapo ripoti itafanya kazi lawama zitakuwa haziepukiki kwake.

Naona timu nyingi zinapambana kutafuta wachezaji ambao wanaona kwamba wanawafaa kwenye kikosi chao kwa ajili ya kuleta ushindani msimu ujao.

Jambo la kuzingatia kwa sasa ni wachezaji makini na wazuri ambao watakuwa na nidhamu nje na ndani ya uwanja hii itasaidia kuwa na benchi makini pamoja na timu imara.

Muda mzuri kwa Shirikiso la Mpira Tanzania (TFF) kuendelea kutoa taarifa mapema na masuala yote yanayohusu usajili kwa wanachama wake kwa wakati huu.

SOMA NA HII  SANE AINGIA ANGA ZA JUVENTUS

IIkumbukwe kwamba kuna timu ambazo zimepanda daraja msimu huu ikiwa ni pamoja na Gwambina FC, Ihefu,Dodoma Jiji hizi zote ni lazima zitambue mfumo unaotumika ndani ya ligi kwa sasa.

Kwa sasa itakuwa vema ikiwa kila mmoja akapewa utaratibu mapema ili baadaye kusije kuwa na sababu kwa timu kushindwa kukamilisha usajili eti kisa walikuwa hawajui utaratibu hio sio sawa kwa kweli.

Kama wachezaji watatukuwa kwenye mazungumzo na timu ni muhimu kuangalia sehemu ambayo wanakwenda pamoja na nafasi yake huko.

Wachezaji wanatambua kwamba wakati huu ni muda wa mauzo hilo lipo wazi lakini lazima wasisahau kwamba kazi yao ni mpira hivyo lazima wacheze.

Wakati wa usajili pia ni muda wa kuonyesha kwamba thamani ya mchezaji uwanjani ilikuaje na nanmna gani anaweza kuwa msaada kule anakokwenda jambo la msingi ni kujitambua.

Ikitokea mchezaji akapata timu na akakubaliana kuwa mchezaji wa hiyo timu anayokwenda basi lazima aendane na utaratibu ambao ataukuta maisha ya mchezaji ambaye hatambua kazi yake ni magumu kwa wakati ujao.

Kila kitu kwenye soka kinawezekana na ipo wazi kwa muda huu malipo ya wachezaji yawe wazi na wajitoe kwa moyo mmoja kufanya kazi na kutafuta matokeo.

Benchi la ufundi litazame namna bora ya kufanya kuweza kusajili wachezaji makini ambao watasajiliwa kupitia ripoti ambazo zimeandaliwa.

Nidhamu inapaswa ipewe kipaumbele na wachezaji wawe makini kuelekea kwenye maisha yao mapya ambayo watakwenda kuanza ni muhimu kuzingatia kwamba maisha yanakwenda kasi sana.

Jambo la msingi kwa viongozi na mabosi wa timu kuzingatia usajili kwa kufuata ripoti na sio mapenzi ya timu ama kiongozi fulani mambo yakiwa hivyo tutaanza kumtafuta mchawi.

Bado kazi ni kubwa katika kujenga timu kwa wakati huu kwani hakuna ambaye hajui kwambasarakasi za usajili zina mambo mengi ndivyo ambavyo inaonekana hali ilivyo kwa sasa.

Achana na hizo sarakasi zinazoendelea maisha lazima yaendelee na ninaamini kwamba ripoti zitafanyiwa kazi na usajili utakuwa bora kwa kuzingatia ripoti, asante sana.