Home Uncategorized KOCHA YANGA: PUMZI TATIZO KWA WACHEZAJI

KOCHA YANGA: PUMZI TATIZO KWA WACHEZAJI

 

KOCHA Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic amesema kuwa tatizo kubwa la wachezaji wake wa Yanga ni kutokuwa na pumzi ya kutosha kutokana na kuwa na maandalizi ya muda mfupi kwa ajili ya msimu mpya wa 2020/21.


Yanga ilianza kukipiga mchezo wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons,  Septemba 6, Uwanja wa Mkapa na ilitoshana nao nguvu kwa kufungana bao 1-1.


Prisons ilianza kupachika bao dakika ya 7 kupitia kwa Lambart Charles ambalo lilisawazishwa na nyota mpya wa Yanga, Michael Sarpong dakika ya 19.


Zlatko amesema kuwa amekitazama kikosi namna kilivyocheza kwa umakini na kugundua tatizo lilikuwa kwenye pumzi kukata mapema jambo lililowapa tabu kupata ushindi.


“Wachezaji wangu wanajituma na wanafanya vizuri, nimegundua kwamba tatizo lipo kwenye pumzi na inatokana na kutokuwa na muda mrefu wa maandalizi, bado tuna muda wa kufanya vizuri hivyo makosa tutayafanyia kazi,” amesema.


Yanga ina kibarua kingine tena Septemba  13 dhidi ya Mbeya City iliyopoteza kwa kufungwa mabao 4-0 na KMC, Uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  KOCHA STARS: MDOGOMDOGO TUNATUSUA CHAN