Home Uncategorized KUWAONA STARS WAKIMENYANA NA BURUNDI BUKU TATU TU

KUWAONA STARS WAKIMENYANA NA BURUNDI BUKU TATU TU

 


SHIRIKISHO la Soka Tanzania,(TFF) limeweka wazi viingilio vya mchezo wa kirafiki uliopo kwenye  ya kalenda ya FIFA utakaoikutanisha timu ya Taifa ya Tanzania dhidi ya Burundi.

Mchezo huo utakaochezwa Oktoba 11,2020, Uwanja wa Mkapa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kasi ya ligi ya Bongo pamoja na ujirani wa nchi hizi za ukanda wa Afrika Mashariki.

Bei elekezi kwa mzunguko ambayo itampa ruhusa shabiki wa Taifa Stars kupata uhondo ni shilingi 3,000(buku tatu) huku VIP B ikiwa ni 10,000 na ile ya VIP A ikiwa ni 20,000.

Pia ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa kwa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Ettiene Ndayiragije ni raia wa Burundi hivyo atakuwa anacheza na timu ambayo anaijua na wao wanaitambua vema mbinu ya mzawa wao. 


Uwepo wa nyota wa Burundi ndani ya ligi ya Bongo ikiwa ni pamoja na Bigirimana Blaise anayekipiga Namungo mwenye mabao mawili msimu huu kwenye ligi Jonathan Nahimana kipa wa Namungo ambaye naye ni imara ndani ya lango vitaongeza ushindani mkubwa.


SOMA NA HII  POLOKWANE FC WAIKOMALIA SIMBA ISHU YA BOCCO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here