Home Uncategorized MARCEL KAHEZA AFICHUA KILICHO NYUMA YA MAFANIKIO

MARCEL KAHEZA AFICHUA KILICHO NYUMA YA MAFANIKIO


 MARCEL Kaheza mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Polisi Tanzania amesema kuwa kikubwa kinachoipa ushindi timu yake ni ushirikiano ambao wanauonyesha wachezaji wakiwa uwanjani pamoja na mbinu za mwalimu.


Polisi Tanzania inafundisha na Malale Hamsini ambaye ni Kocha Mkuu, mchezo wake uliopita wa raundi ya nne ilishinda mabao 3-0 mbele ya Dodoma Jiji mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kaheza anashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye raundi ya nne ambapo alifunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Dodoma Jiji.

Nyota huyo amesema:”Mwalimu amekuwa akitupa mbinu nyingi kwa ajili ya kutafuta ushindi nasi pia tumekuwa tukizifuata, sapoti kutoka kwa mashabiki na ushirikiano ambao tunaupata ni jambo ambalo linatupa ushindi.”


Mchezo wao unaofuata kwa Polisi Tanzania ni Oktoba 5, Uwanja wa Uhuru itakuwa dhidi ya KMC ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar.

SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA CHATUA SALAMA ZANZIBAR, LAMINE 'OUT'