Home Uncategorized YANGA: MPIRA SIO UADUI, MUHIMU KUENDELEZA UPENDO

YANGA: MPIRA SIO UADUI, MUHIMU KUENDELEZA UPENDO

 




UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa ni muhimu mashabiki wake wakaelewa kwamba mpira sio uadui bali ni mwendelezo wa upendo na mshikamano katika kila jambo ambalo wanalifanya hivyo ni muhimu kwao kuacha kabisa tabia hiyo.


Septemba 27 wakati Yanga ikishinda bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, baadhi ya mashabiki wa Yanga walionekana kuleta vurugu jambo ambalo limekemewa vikali na Yanga wenyewe, Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) pamoja na wadau wa masuala ya mpira.


Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa kwa sasa elimu inaendelea kutolewa kwa mashabiki pamoja na wadau wa mpira ili kuweza kuondoa kabisa tatizo hilo.

“Mashabiki wa Yanga wanapaswa waelewe kwamba mpira sio uaduia ni furaha na mshikamano, kwa sasa elimu inazidi kuendelea kutolewa lengo ikiwa ni kupunguza na kuondoa kabisa hili tatizo.


“Kwa mashabiki wa Simba, Yanga sisi sio maadui bali tunafanya ule utani wa jadi, jukumu ni letu pia tuna kazi ya kufanya kama ilivyokuwa zamani ambapo utani ulikuwa ni kwenye mpira pekee ila upendo unadumu huku kwenye shida wakiwa pamoja ikiwa ni kwenye misiba hivyo muhimu kuendeleza utamaduni,” amesema.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII KWA SASA