Home Uncategorized AISHI MANULA WA SIMBA ANA KAZI YA KUFANYA KWA VITA YA REKODI

AISHI MANULA WA SIMBA ANA KAZI YA KUFANYA KWA VITA YA REKODI

 


AISHI Manula, kipa namba moja ndani ya Klabu ya Simba kwa sasa kichwa kinampasuka kila anapotazama namna makipa wenzake wanavyoandika rekodi mpya huku naye akiwa na kazi ya kupambania gloves zake za kipa bora alizopewa msimu wa 2019/20.

Kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara ukiachana na vita ya kiatu cha ufungaji bora pia kwa upande wa makipa mambo yanazidi kupamba moto ambapo kinara ni David Kissu wa Azam FC akiwa nazo sita kati ya mechi saba na amefungwa mabao mawili.

 
Nafasi ya pili ipo mikononi mwa Aron Kalambo wa Klabu ya Dodoma Jiji FC ya Mbwana Makata akiwa nazo sita kati ya mechi saba ambazo amecheza na amefungwa mabao matatu ambapo alifungwa na timu ya Polisi Tanzania.


Metacha Mnata wa Yanga naye yupo pia akiwa amekaa langoni mechi tano kati ya sita ambazo Yanga imecheza na hajafungwa kwenye hizo mechi tano ambazo alikaa langoni.

Daniel Mgore wa Biashara United naye ana biashara yake kwani ana clean sheet tano kati ya mechi saba ambazo amekaa lango akiwa amefungwa mabao saba kwenye mechi mbili ambazo alifungwa na Simba mabao manne na Coastal Union mabao matatu.

Mtetezi wa gloves Manula yeye yupo zake na clean sheet tatu kati ya mechi sita ambazo amekaa langoni akifungwa jumla ya mabao matatu akiwa langoni. 

Manula ametunguliwa bao mojamoja kwenye timu tatu mbele ya Ihefu, Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons.

SOMA NA HII  POFBA APIGWA STOP MAN UNITED