Home Uncategorized KINARA WA UTUPIAJI BONGO AIKACHA TUZO YA KAGERE

KINARA WA UTUPIAJI BONGO AIKACHA TUZO YA KAGERE

 


KINARA wa chati ya ufungaji Bongo, Mzimbabwe Prince Dube ameibuka na kubainisha kwamba akili yake ni kuendelea kufunga mabao ambayo yataifanya klabu yake kuwa mabingwa wa ligi na siyo kutwaa kiatu cha ufungaji bora.

 

Dube ameongeza kwamba akili yake ni kuendelea kufunga mabao kwa ajili ya timu yake huku suala la kuwa mfungaji bora akiliweka mwishoni mwa msimu.

 

Mzimbabwe huyo kwa sasa ndiye kinara wa ufungaji Bara akiwa na mabao matano akifuatiwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere mwenye mabao manne.


Dube amesema kuwa kwa sasa hana mawazo na kuwa mfungaji bora kwa sababu ya kujitolea kwa ajili ya timu yake kufikia malengo yao ya kuwa mabingwa.

 

“Kuhusu suala la kuwa mfungaji bora kwa wakati huu hapana kwa sababu nafanya majukumu kwa ajili ya timu.

 

“Mabao ninayoyafunga nataka yaisaidie timu kufikisha malengo yake ya kuwa mabingwa tofauti na mimi kuwa mfungaji bora na kama ikiwa hivyo basi iwe mwishoni mwa msimu,” amesema.


Azam FC ina kazi ya kucheza na Mwadui FC iliyotoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Namungo FC, Novemba 15 Uwanja wa Azam Complex.


Wenyewe Azam FC wametoka kushinda kwa mabao 4-2 dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa raundi ya tano uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.


Ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 15 inakutana na Mwadui FC iliyo nafasi ya nane na pointi zake sita.

 

Msimu uliopita Kagere alichukua tuzo hiyo kwa kufanikiwa kufunga mabao 22.

SOMA NA HII  YANGA WATAJA MBINU ITAKAYOWAPA UBINGWA WA LIGI KUU BARA