Home Uncategorized YANGA WATAJA MBINU ITAKAYOWAPA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

YANGA WATAJA MBINU ITAKAYOWAPA UBINGWA WA LIGI KUU BARA


 BAADA ya kukaa kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, ameibuka na kuwaambia wachezaji kuwa kama wanataka kutimiza malengo yao ya kuchukua ubingwa, basi wasitoke katika nafasi hiyo ya kwanza waliyopo.

 

 

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 31 inafuatiwa na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 26 zote zimecheza mechi 13 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 23 baada ya kucheza mechi 11.


Katika michezo miwili iliyopita ya ligi waliyocheza dhidi ya Azam FC na ule na JKT Tanzania, Yanga kila mmoja ilipata ushindi wa bao 1-0, yaliyofungwa na Deus Kaseke.

 

Kaze amesema kuwa amefanya kikao na wachezaji wake mara baada ya mchezo dhidi ya JKT akiwataka kuendelea na kasi hiyo waliyoianza katika mzunguko wa kwanza kabla ya kwenda wa pili.

 

Kaze amesema katika siku saba zilizopita walikuwa na ratiba ngumu ya kucheza michezo mitatu mfululizo na kufanikiwa kupata pointi saba kati ya tisa ambazo siyo mbaya kwao kutokana na ugumu wa timu ambazo wamekutana nazo.

 

“Bado tunaendelea kuimarisha timu wachezaji wanapambana sana kuhakikisha timu inabaki kukaa kileleni, kwani malengo yetu ni kuendelea kuongoza hadi mwishoni mwa ligi, hii tu ndiyo mbinu inayoweza kutupa ubingwa.

 

“Michezo mitatu ndani ya siku saba hakuna mwili wa mchezaji unaweza kuhimili mchakamchaka huo, hivyo niwapongeze wachezaji wangu kwa kupambana kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki wao,” .

SOMA NA HII  BOSI SIMBA ATUMA UJUMBE KWA KOCHA, WACHEZAJI KISA YANGA