Home Uncategorized KUMBE ISHU YA KOCHA MPYA YANGA TFF ‘WABUMISHA’

KUMBE ISHU YA KOCHA MPYA YANGA TFF ‘WABUMISHA’

 


KUFUATIA Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutangaza kusogeza mbele mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga ‘Kariakoo Dabi’ kumesababisha kumchelewesha kocha mpya wa Yanga, Cedric Kaze ambaye alitakiwa kutua jana Alhamisi, sasa atatua kesho leo Jumamosi au Alhamisi ijayo.

 

Simba na Yanga zilikuwa zikutane Oktoba 18 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ambapo kwa sasa zitakutana Novemba 7 kutokana na sababu ya changamoto ambazo zimetajwa ni kuhusu tahadhari ya Corona kwa wachezaji wa kimataifa.

 

Yanga imeshamalizana na Kaze ambaye anakuja kubebe mikoba ya Mserbia, Zlatko Krmpotic tayari kwa ajili ya kuanza kukinoa kikosi hicho baada ya kutanguliza majembe yake ya ushindi.


Taarifa kutoka katika benchi la ufundi la Yanga zinasema kuwa, Kaze anatarajia kutua rasmi kuanza kuitumikia timu hiyo Alhamisi ijayo huku akiwa anaweka mipango yake sawa kabla ya kutua klabuni hapo.

 

“Awali alikuwa atue Alhamisi hii ili kujiandaa na mchezo wa Simba, ilikuwa lazima awahi kujiandaa na mchezo huo muhimu.


“Hivyo, baada ya kuahirishwa kwa mechi hiyo, sasa anamalizia mipango yake ili akija awe kamili kuanza kazi ya kuitumikia Yanga,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Pamoja na ripoti hiyo, taarifa nyingine zilieleza kuwa kocha huyo anaweza kuingia Dar, leo Jumamosi kama baadhi ya mambo yataenda sawa kama ambavyo mwenyewe amekuwa akipanga.

SOMA NA HII  TAKUKURU YABAINISHA KINACHOENDELEA ISHU YA BILIONI MOJA YA MAGUFULI KWA AJILI YA AFCON