Home Uncategorized KUMBE KAZE ALIKUWA KWENYE HESABU ZA SIMBA

KUMBE KAZE ALIKUWA KWENYE HESABU ZA SIMBA

 


IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Yanga wa sasa, Cedric Kaze alikuwa kwenye hesabu za mabosi wa Simba baada ya kumchimbisha Patrick Aussems kwenye nafasi hiyo msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na Sven Vandenbroeck.

Sven ambaye aliikuta timu ikiwa inaongoza ligi aliendelea pale ambapo Aussems maarufu kama Uchebe alikuwa ameishia na alifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho na kwa msimu huu ameanza kutwaa  taji la Ngao ya Jamii.

Mshauri Mkuu wa Klabu ya Yanga kuelekea kwenye mabadiliko, Senzo Mbatha anatajwa kuwa alikuwa akisimamia kila kitu kuhusu Kaze kuibukia Simba wakati alipokua Mtendaji Mkuu ndani ya Simba ila dili hilo lilikwama na wakampata Sven.


Kwa sasa Mbatha anafanya kazi ndani ya Yanga akiwa ni mshauri na ameweka wazi kuwa sababu kubwa ya kuibukia ndani ya klabu hiyo ni kuona kwamba anafanya kazi na timu yenye malengo ya kufikia mafaniko jambo ambalo analiona.


Kaze ameanza kuinoa Yanga na amekiongoza kikosi hicho kwenye mechi mbili na kuvuna pointi sita na kikosi chake kipo nafasi ya pili na pointi 19 baada ya kucheza mechi saba.


Kwa sasa kinajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 31, Uwanja wa Karume.


SOMA NA HII  MECHI YA SIMBA NA MTIBWA YAPANGULIWA, RATIBA MPYA YATAJWA