Home Uncategorized RUVU SHOOTING: TULIWAAMBIA SIMBA MAPEMA KWAMBA TUTAWAPAPASA, WALIPUUZA

RUVU SHOOTING: TULIWAAMBIA SIMBA MAPEMA KWAMBA TUTAWAPAPASA, WALIPUUZA


OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa aliwapa tahadhari mapema wapinzani wake Simba kabla ya kukutana nao uwanjani jambo ambalo walilipuuzia awali.


Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Oktoba 26, Uwanja wa Uhuru Simba ilikubali kichapo cha bao 1-0 na kuyeyusha pointi tatu wakiwa nyumbani.


Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa taarifa za kuwapapasa alizitoa mapema ila walimpuuzia.


” Niliwaambia mapema kuwa mpira tunaocheza Ruvu Shooting ni kama Barcelona ya Bongo, wao walifikiri ni porojo wakataka kulipa kisasi kwetu hilo walilikosea.

 “Simba walikuwa wanasema wanacheza pira biriani nadhani sasa litakuwa pira kachori maana kwa mpira ambao tumecheza pale ni kidogo sana hatukuwa kwenye ule ubora wetu ambao tumeuzoea nadhani ni mwanzo tu tutaendelea kuwakung’uta na kuwapapasa, ” amesema.


Mabingwa watetezi Simba wamepoteza mechi mbili mfululizo kwa msimu wa 2020/21 walianza kuchapwa na Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela bao 1-0 na mchezo wa pili walinyooshwa na Ruvu Shooting bao 1-0. 


SOMA NA HII  KISA KICHAPO MBELE YA SIMBA, KOCHA AWACHANA WACHEZAJI WAKE JUU YA KIWANGO