Home Uncategorized KISA KICHAPO MBELE YA SIMBA, KOCHA AWACHANA WACHEZAJI WAKE JUU YA KIWANGO

KISA KICHAPO MBELE YA SIMBA, KOCHA AWACHANA WACHEZAJI WAKE JUU YA KIWANGO

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa wachezaji wake hawakucheza vizuri kwenye mchezo wao wa jana dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Simba ilishinda kwa bao 1-0 na kuwafanya Kagera Sugar kuacha pointi zote sita mbele ya Simba msimu huu wa 2019/20 baada ya ule wa kwanza kufungwa mabao 3-0 Uwanja wa Kaitaba.

“Wachezaji wangu walionyesha kiwango cha kawaida sio kile ambacho nimekizoea ila wamepambana kutafuta matokeo mambo yakawa magumu kwao  ni sehemu ya mchezo makosa yaliyojitokeza tutayafanyia kazi,” amesema.

Kagera Sugar imefungwa jumla ya mabao manne msimu huu na Simba, kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Kaitaba ilifungwa mabao 3-0 na jana ilifungwa bao 1-0.

SOMA NA HII  POCHETTINO ACHEKELEA KUPATA KAZI