Home Uncategorized SIMBA KUCHEZA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI

SIMBA KUCHEZA MECHI MBILI ZA KIRAFIKI

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo kikosi kimeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zake za Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za kirafiki.


Oktoba 18 ilikuwa ni dabi kati ya Yanga na Simba imepelekwa mbele mpaka Novemba 7 na Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) leo Oktoba 7.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwa sasa timu imesharejea kambini na wachezaji wale ambao hawajaitwa kwenye timu zao za taifa wanajiandaa kwa ajili ya mechi za ligi na kirafiki.

Miongoni mwa wachezaji ambao hawajaitwa timu ya zao za taifa ni Bernard Morrisons, Ibrahim Ajibu, Miraji Athuman, Pascal Wawa.

“Timu inajiandaa na mechi nyingine za ligi hasa baada ya mchezo wetu wa dabi dhidi ya Yanga kupelekwa mbele sisi hatuna cha kusema katika hilo kazi yetu ni kucheza.  

“Kwa namna ambavyo tumejipanga tutacheza mechi mbili za kirafiki ambapo moja itakuwa ni Oktoba 10 tutacheza mechi ya kirafiki na Pan Africa halafu baadaye tutacheza mechi nyingine na Mlandege.

“Tunaendelea kujipanga kwa ajili ya mechi nyingine na timu ipo tayari kwa ajili ya kupambana masuala ya ratiba wenye mamlaka wanajua namna ya kupanga,” amesema.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA ACHUKIZWA NA MORRISON, AMCHANA YONDANI - VIDEO