NYOTA wa Azam FC wanaingia kwenye vita ya kuwania tuzo ya mwezi Septemba na Oktoba baada ya uongozi wa matajiri hao wa Dar es Salaam kuamua kuanzisha tuzo hiyo.
Miongoni mwa mastaa ambao wapo kwenye orodha ya kuwania tuzo hiyo ni pamoja na mtupiaji namba moja Bongo, Prince Dube mwenye mabao sita na Obrey Chirwa mwenye mabao manne.
Wengine ni pamoja na Salum Abubakary,’Sure Boy’ ambaye yeye ametupia bao moja na ana pasi moja ya bao ndani ya kikosi hicho kilicho nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zake kibindoni ni 22.
Kipa wao namba moja David Kissu pia yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowania tuzo hizo akiwa ana jumla ya clean sheet saba kibindoni baada ya kukaa langoni kwenye mechi tisa kwa msimu wa 2020/21.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mchakato wa kurejesha tuzo hizo umekamilika na kwa sasa wataanza kwa wachezaji ambao wamefanya vizuri mwezi Septemba na Oktoba.
Ameweka wazi kuwa utoaji wa tuzo hizo ulikuwepo kipindi cha nyuma ila ulisisimama baada ya wadhamini kusepa kwenye mchakato huo.