Home Uncategorized ISHU YA NYOTA WAWILI KUTAKIWA NA TP MAZEMBE UONGOZI WA YANGA WACHEKELEA

ISHU YA NYOTA WAWILI KUTAKIWA NA TP MAZEMBE UONGOZI WA YANGA WACHEKELEA


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa suala la wachezaji wake wawili wazawa kudaiwa kuwa wanawaniwa na Klabu ya TP Mazembe linawapa matumaini ya kuamini kwamba timu yao inafuatiliwa na watu wengi duniani.


Feisal Salum pamoja na Bakari Mwamnyeto ambao wapo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachocheza kesho, Novemba 13 dhidi ya Tunisia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2021 nchini Cameroon wamekuwa wakitajwa kuingia anga za TP Mazembe ya Congo.


Nyota hao wamekuwa kwenye ubora wao kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara wakiwa na uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza kinachonolewa na Cedric Kaze.


Mwamnyeto ambaye ni beki ameshuhudia mabao matatu yakitikisa nyavu za timu yake kwenye mechi 10 ikiwa ni timu iliyofungwa mabao machache ndani ya ligi.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa hawashangazwi na taarifa hizo kwa kuwa wachezaji wao ni bora na wana uwezo mkubwa.


“Ipo wazi kwamba tuna kikosi kizuri na chenye wachezaji makini hivyo wachezaji wetu kutakiwa na TP Mazembe naona sio jambo mbaya hivyo ofa ikija mezani basi tutajua tutafanyaje, na hii inamaanisha kwamba kikosi chetu kinafuatiliwa duniani” amesema. 

SOMA NA HII  MCHEZO WA KIRAFIKI: SIMBA 0-0 AFRICAN LYON