Home Uncategorized MASHABIKI WAITWA UWANJA WA MKAPA KESHO KUISAPOTI STARS SAA 4 USIKU

MASHABIKI WAITWA UWANJA WA MKAPA KESHO KUISAPOTI STARS SAA 4 USIKU


 MJUMBE wa Kamati ya Ushindi wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Haji Manara amesema kuwa linapofika suala la kushabikia Stars muhimu kuweka kando tofauti za mashabiki.


Kesho Stars itakuwa na mchezo wa pili dhidi ya Tunisia ambazo zote zipo kundi J baada ya ule wa kwanza Stars kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Kwenye kundi J katika harakati za kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon, Tunisia ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi tisa huku Stars ikiwa na pointi tatu kibindoni na ipo nafasi ya nne.

Manara amesema kuwa inapofika wakati wa masuala ya Taifa la Tanzania huwezi kugawa kwa itikadi ama klabu yoyote ile.

“Tusiufanye mpira kuwa itikadi yaani kila mmoja anataka kuwa na timu yake ila inapofika suala la timu ya Taifa hapo lazima tuwe kitu kimoja.


“Huwezi kuacha kula ubwabwa na watu wa Yanga, kisa upo Simba ama Yanga lakini inapofika suala la timu ya Taifa ni kwamba lazima tuwe kitu kimoja hasa ukizingatia kwamba tutakuwa nyumbanii.


“Kuna jezi nyingi za timu ya Taifa na kila mmoja aje akiwa amevaa jezi yake na kuna rangi nyingi ikiwa ni pamoja na ile ya njano, nyeupe na nyeusi hizi zote ni jezi zetu wote kila mmoja avae jezi yake,” amesema.


Stars itacheza kesho Uwanja wa Mkapa saa 4 usiku na mashabiki watakaoruhusiwa kuingia ni asilimia 50 kutokana na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kutoa maelekezo hayo kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.



 

SOMA NA HII  SIMBA WAPEWA MAMILIONI YA KUTOSHA NA SportPesa