Home Uncategorized MUUAJI WA AL RABITA FURAHA YAKE IPO HAPA

MUUAJI WA AL RABITA FURAHA YAKE IPO HAPA

 


STEPHEN Sey nyota wa Namungo FC amesema kuwa furaha yake ni kuona timu inapata matokeo ndani ya Uwanja jambo ambalo lilimfanya jana Novemba 28 kutupia mabao mawili wakati timu yake ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Al Rabita FC ya Sudan Kusini.


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ulikuwa ni wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho ambapo kwa Tanzania inawakilishwa na Namungo FC.


Ikiwa ni mara ya Kwanza kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kupanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20  imeanza kwa ushindi jambo linalotoa matumaini ya kupata nafasi ya kusonga mbele.


Mabao hayo alipachika kipindi cha Kwanza dakika ya 20 na 39 na bao moja lilipachikwa na Shiza Kichuya dakika ya 64.


Sey amesema;”Furaha yangu ni kuona timu inapata matokeo chanya hakuna kingine zaidi ya hilo hivyo tunawashukuru mashabiki kwa sapoti yao wazidi kutupa sapoti, “

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO