Home Uncategorized VIWANJA SABA VYAPIGWA PINI NA BODI YA LIGI

VIWANJA SABA VYAPIGWA PINI NA BODI YA LIGI

 


BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) leo Novemba 2 imevifungia viwanja viwanja 7 kutotumika kwa ajili ya mechi za mashindano kutokana na kukosa baadhi ya  sifa za kikanuni zilizoanishwa zinazozungumzia sheria namba 1 ya mpira.


Viwanja hivyo ambavyo vimepigwa pini ili vifanyiwe marekebisho na TPLB itavikagua baada ya marekebisho kukamilika ni pamoja na :-


Uwanja wa Majimaji uliopo Songea ambao ulikuwa unatumika na Klabu ya Majimaji.


Uwanja wa Sabasaba wa Njombe ambao ulikuwa unatumiwa na Klabu ya Njombe Mji.


Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi wa Tabora.


Uwanja wa Mkwakwani Tanga ambao ulikuwa unatumika na Klabu ya Coastal Union ya Tanga.


Uwanja wa Kipiji wa Mbeya.


Uwanja wa Nangwanda Sijaona wa Mtwara, uliokuwa unatumiwa na Ndanda FC.


Uwanja wa Jamhuri wa Dodoma ambao ulikuwa unatumiwa na JKT Tanzania.


TPLB imeelekeza maeneo yafuatayo yafanyiwe kazi:-

Marekebisho eneo la kuchezea,(pitch).

Maeneo ya kukaa wachezaji wa akiba na benchi la ufundi.


Vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji.  

SOMA NA HII  MANULA:TUTAFANYA VIZURI KIMATAIFA