Home Uncategorized AZAM FC YAWAITA MASHABIKI AZAM COMPLEX KUONA BURUDANI

AZAM FC YAWAITA MASHABIKI AZAM COMPLEX KUONA BURUDANI


UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upa tayari kwa mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho hatua ya tatu dhidi ya Magereza FC.


Mabingwa watetezi wa taji la Kombe la Shirikisho ni Simba ambao walitwaa msimu wa 2019/20 mikononi mwa Azam FC ambayo haikuambulia taji lolote.

Leo, Desemba 26 inawakaribisha Magereza Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yalianza Deemba 23 hivyo leo wanakamilisha kazi ambayo walikuwa wanahitaji kuifanya.

“Maandalizi yalianza muda mrefu na leo tunaamini kwamba vijana wetu watafanya kile ambacho tulikuwa tunahitaji kukifanya.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi ndani ya uwanja kuipa sapoti timu yao kwani unapigwa mpira mwingi na matokeo yataonekana,” .
SOMA NA HII  ORODHA YA WACHEZAJI WA SIMBA WATAKAOIFUATA PLATEAU UNITED YA NIGERIA KIMATAIFA