Home Uncategorized CRISTIANO RONALDO: BARCELONA HAIFANYI VIZURI

CRISTIANO RONALDO: BARCELONA HAIFANYI VIZURI

 


STAA wa Juventus, Cristiano Ronaldo amefunguka yeye si mpinzani wa Lionel Messi ila ni rafiki yake na wamekuwa na uhusiano mzuri huku akiweka wazi kuwa anaona timu hiyo siku za hivi karibuni haifanyi vizuri.

 

Desemba 8, Ronaldo alikutana na Messi kwa mara nyingine kwenye Uwanja wa Camp Nou katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Barcelona na Juventus.


 Juventus iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku mabao mawili yakifungwa na Ronaldo kwa njia ya penalti.


Ronaldo alirudi Hispania kwa mara ya kwanza hivi karibuni kucheza tangu aondoke Real Madrid, lakini amewahi kucheza dhidi ya Valencia na Atletico Madrid akiwa mchezaji wa Juventus.

 

“Tumekuwa na uhusiano mzuri kwa kipindi chote na Messi. Sio ni kama ni mpinzani wangu. Kila mmoja wetu amekuwa katika ubora wake hasa akiwa na timu yake jambo ambalo ni zuri.


 “Nimefurahia kurudi tena Hispania hasa hapa Catalonia.Imekuwa ngumu kucheza ndani ya Camp Nou tena dhidi ya timu bora ambayo imekuwa si rahisi kupambana nayo.


“Lakini tumecheza kama timu kwa hiyo sisi ni washindi na mabingwa wa familia moja kwani jinsi tulivyocheza hakuna cha kutukwamisha zaidi kuongeza bidii na kufika mbali.

 

“Kama unafunga mabao matatu hapa Camp Nou basi ni wazi unastahili kumaliza nafasi ya kwanza. Ingawa naona Barcelona kwa sasa haifanyi vizuri,” amesema Ronaldo.

SOMA NA HII  KILICHOIKWAMISHA YANGA KUPATA SAINI YA BEKI KUTOKA KMC CHATAJWA