Home Uncategorized FAMILIA YAMUONDOA KIKOSINI MZAMBIA WA SIMBA

FAMILIA YAMUONDOA KIKOSINI MZAMBIA WA SIMBA

 


RARRY Bwalya, kiungo wa Simba raia wa Zambia kesho kunahatihati ya kuukosa tena mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City kutokana na matatizo ya kifamilia.


Raia huyo wa Zambia aliukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara Desemba 9 dhidi ya Polisi Tanzania wakati Simba ikishinda mabao 2-0 yote yalifungwa na mshkaji wake Clatous Chama. 


Alisepa Bongo na kuibukia Zambia baada ya kupewa ruhusa na mabosi wake wa Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck akishirikiana na msaidizi wake Seleman Matola. 


Vandenbroeck amesema kuwa Bwalya atàkuwa nje ya kikosi kwa muda mpaka pale masuala yake yatakapokuwa sawa.


“Bwalya ana matatizo ya kifamilia atakuwa huko kwa siku kadhaa na atarudi pale tu masuala hayo yatakapokwisha, ila uzuri ni kwamba wengine wapo kwa ajili ya mechi hizi za ligi,’.


Kiungo huyo alikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza kwenye Dar Dabi dhidi ya Yanga iliyochezwa Uwanja wa Mkapa iliyokamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 Novemba 7.

SOMA NA HII  Salimu Aiyee na kiboko ya Simba Sc wapo mtegoni.