Home Uncategorized ISHU YA MORRISON KUTAKIWA KULIPA MKWANJA KESI YAKE CAS YALETA KIGUGUMIZI

ISHU YA MORRISON KUTAKIWA KULIPA MKWANJA KESI YAKE CAS YALETA KIGUGUMIZI


AMRI Kiemba, kiungo aliyecheza kwa mafanikio ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kabla ya hivi karibuni kuamua kutundika daluga amesema kuwa suala la Bernard Morrison kuchanga ili kesi yake isikilizwe halimuingii akilini.

Kiemba pia amewahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba, Yanga na Ruvu Shooting na kote alikuwa ni chaguo la kwanza la walimu aliokuwa akifundishwa nao.

Kwa sasa Kiemba anasimamia kituo cha kukuza vipaji kwa watoto kilichopo Mabibo, Dar.

Nyota huyo amesema kuwa sakata la Morrison kwa uelewa wake kwenye suala la mchezaji huyo kutakiwa pia kulipa faini ili kesi yake isikilizwe halimuingii akilini.

“Kwa ufahamu wangu mdogo kwa mambo ya kesi linapokuja ishu ya kulipia anayepaswa kulipa ni yule anayekwenda kushtaki na siyo mshatikwa.

“Anayeshtaki ndiye anapaswa kulipa masuala ya kesi sasa kwa namna ilivyo kwamba anayeshtakiwa naye anatakiwa kulipa bado hainiingii akilini,” .

Morrison anashtakiwa na Yanga kuhusu sakata lake la mkataba wake ambapo yeye anadai kwamba alisajiliwa kwa muda wa miezi sita ndani ya Yanga.

Yanga ambao wanamshtaki wanadai kwamba ana dili la miaka miwili hivyo bado ni mchezaji wao halali ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Cedric Kaze.

Hivi karibuni Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela aliweka wazi kwamba wameambiwa na mahakama ya usuluhishi,(Cas) kwamba wanatakiwa kulipa fedha wote wawili, mchezaji na wao ili kesi yao isikilizwe.

SOMA NA HII  VIDEO: DIAMOND ATUA NA HELKOPTA KAHAMA