Home Uncategorized KOCHA YANGA: NTIBAZONKIZA HANA KAZI YA KUFUNGA

KOCHA YANGA: NTIBAZONKIZA HANA KAZI YA KUFUNGA

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze raia wa Burundi ameweka bayana kwamba staa wake mpya Saidi Ntibazonkiza hatakuwa na kazi ya kufunga mabao kwani ana majukumu maalum ambayo amempatia ayafanye akiwa uwanjani.

 

Kaze amefunguka kuwa majukumu aliyompa Ntibazonkiza ni kuhakikisha anatumia uzoefu wake wa kucheza soka Ulaya kwa ajili ya kuongeza ari kwa washambuliaji wake kwa ajili ya kufunga mabao katika mechi za kikosi hicho.

 

Ntibazonkiza ambaye ameanza mazoezi na Yanga kwa mara ya kwanza ataanza kuitumikia Yanga kuanzia Desemba 15, baada ya kusajiliwa kama mchezaji wa dirisha dogo.


Kaze amesema anataka kutumia uzoefu wa Ntibazonkiza wa kucheza Ulaya kwa zaidi ya miaka 15 kuwa chanzo kikuu cha kuvuna mabao ndani ya kikosi hicho.

 

“Saidi amecheza soka la profesheno Ulaya kwa zaidi ya miaka 15 tena kwenye timu kubwa, amekuja kutuongezea hali ya kujiamini kwa wachezaji wengine.


“Siyo atakuja kufunga mabao tu, hapana bali atakuja kuwafanya wale ambao anacheza nao kujiamini zaidi na kuongeza kupambana kwenye suala la kufunga.


“Hatufungi mabao siyo kwamba timu ni mbovu, hapana ila kuna muda wachezaji hawajiamini hivyo Ntibazonkiza atakuja kuinua hali yao na tutafunga zaidi,” amesema.


Yanga ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 14 imefunga jumla ya mabao 17 na ina pointi 34 kibindoni.


Kinara wa utupiaji ndani ya kikosi hicho ni Michael Sarpong mwenye mabao manne.

SOMA NA HII  COUNTINHO KUBAKI BAYERN MUNICH MSIMU UJAO UWEZEKANO NI MDOGO KWELI