Home Uncategorized MBELGIJI WA SIMBA AWACHARUKIA WACHEZAJI WAKE

MBELGIJI WA SIMBA AWACHARUKIA WACHEZAJI WAKE


 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji amecharuka na kuwataka wachezaji wake kucheza kwa kujituma kuelekea kwenye mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.

Simba ilipoteza mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya FC Platinum uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe kwa kufungwa bao 1-0 lililopachikwa na Perfeck Chikwende.

Ina kibarua cha kupindua meza Uwanja wa Mkapa unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Januari 6, ambapo Ofisa Habari wa timu hiyo Haji Manara amesema kuwa utakuwa ni mchezo wa vita ndani ya Dar.

Vandenbroeck amesema kuwa kilichowaponza washindwe kushinda mchezo huo ni kukosekana kwa umakini kwa wachezaji wake jambo ambalo limemkasirisha hasa hivyo hatapenda kuona makosa yanajirudia.


“Tuliweka wazi malengo yetu tangu awali kwamba ni lazima tuweze kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika. Kuanza kwa kupoteza hiyo ni mbaya kwetu na haijanifurahisha hasa kwa kuwa mchezo tuliweza kuumiliki ila umakini ulikosekana.

“Kwenye mchezo wetu wa marudio hatuna chaguo la kufanya zaidi ya kutafuta matokeo chanya na wachezaji kujituma zaidi, hivyo mashabiki watupe sapoti tunaamini kwamba tutafanya vizuri,” amesema Vandenbr.oeck.

SOMA NA HII  NOMA!! HUU NDIYO UBALAA WA MIPANGO YA YANGA MSIMU UJAO - VIDEO