Home Uncategorized MIKAKATI YA AZAM FC KWENYE USAJILI YAWEKWA WAZI

MIKAKATI YA AZAM FC KWENYE USAJILI YAWEKWA WAZI


 KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina amesema kuwa katika kuhakikisha mipango ya kutwaa ubingwa kwa timu hiyo inatimia, atakaa na uongozi wa timu hiyo ili kujua mchezaji wa kumsajili kwenye dirisha dogo.

 

Lwandamina ambaye alijiunga na Azam hivi karibuni akichukua mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Aristica Cioaba, tayari amekaa kwenye benchi katika mechi mbili.


Alianza kwenye mchezo dhidi ya Namungo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na iliisha sare ya mabao 2-2.


Kisha ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Azam Complex ulikamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.


Azam FC kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa imevuna pointi 29 baada ya kucheza mechi 16,

 

 Lwandamina amesema: “Hakuna kitu chochote ambacho nitaahidi kwa sasa kuhusu usajili lakini nitakaa na mkurugenzi kwa ajili ya kujua ni kitu gani nitakifanya kwenye kipindi hiki cha usajili.

 

“Kila siku kuna ushindani mkubwa ambao pia unachangia ligi kuwa ngumu na bora, na ligi ya Tanzania kwa sasa imezidi kuwa kubwa kwani watu wanafikiwa na taarifa popote walipo tofauti na zamani,” .

SOMA NA HII  MANARA: STARS HAIWEZI KUCHUKUA UBINGWA - VIDEO