Home Uncategorized MUUAJI WA SIMBA KIMATAIFA AINGIA ANGA ZA AZAM FC

MUUAJI WA SIMBA KIMATAIFA AINGIA ANGA ZA AZAM FC


 IMEELEZWA kuwa nyota wa Klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe, Perfect Chikwende yupo kwenye hesabu za mabosi wa Klabu ya Azam FC.


Jina la Chikwende kiungo wa FC Platinum ghafla limekuwa maarufu ndani ya ardhi ya Bongo baada ya kuwatungua Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa.

Desemba 23, Simba ikiwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ilipoteza mchezo huo kwa kufungwa bao 1-0 na mtibuaji mipango akiwa ni nyota huyo dakika ya 17.

Kiungo huyo mwenye miaka 27 amesema kuwa anaweza kujiunga na Azam FC ikiwa timu yake haitasinda mbele kwenye mashindano hayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikiwa FC Platinum itasonga mbele basi itakuwa ngumu kwa Azam FC kumpata kwa msimu huu kwa sababu dirisha dogo litakuwa limefungwa mpaka muda wa mechi za hatua ya makundi zitakaponza kuchezwa.


Habari zimeeleza kuwa nyota huyo amewekwa kwenye rada za mabosi wa Azam FC ili kuongeza makali kwenye safu ya kiungo inayoongozwa na Salum Abubakar, ‘Sure Boy’.


SOMA NA HII  HAZARD: NIMEFANYA JAMBO GUMU MAISHANI KUONDOKA CHELSEA