Home Uncategorized ORODHA YA NYOTA WATANO SIMBA WATAKAOTOLEWA KWA MKOPO

ORODHA YA NYOTA WATANO SIMBA WATAKAOTOLEWA KWA MKOPO


NYOTA watano wa Klabu ya Simba wanatajwa kuwekwa kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo ili wakapate changamoto mpya.


Hivi karibuni Mtendaji wa Simba,  Barbara Gonzalez aliweka wazi kwamba wapo nyota ambao watatolewa kwa mkopo ndani ya Simba.

Nyota wanaotajwa kuwa kwenye hesabu za kutolewa kwa mkopo ni pamoja na kiungo Ibrahim Ajibu ambaye hana nafasi kikosi cha kwanza chini ya Sven Vandenbroeck.

Miraji Athuman pia anatajwa kuwekwa kwenye mpango huo ili wakapate changamoto mpya.

Kened Juma, Ibrahim Ame ambao ni mabeki nao wamewekwa kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo.

Mshambuliaji namba nne wa Simba, chaguo la Sven kwenye usajili kwenye Charles Ilanfya kutoka KMC yeye mapema tu aliomba kuondolewa kwa mkopo kwa kuwa amecheza dakika 62 ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons. 
SOMA NA HII  AZAM FC WATIA TIMU MARA KWA WANAJESHI WA MPAKANI