Home Uncategorized POGBA ATAKIWA KUMFUTA KAZI WAKALA WAKE

POGBA ATAKIWA KUMFUTA KAZI WAKALA WAKE


 KIUNGO wa zamani wa Man United ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka katika kituo cha BT Sport, Paul Scholes, ameeleza kuwa Paul Pogba anatakiwa kumzuia wakala wake, Mino Raiola, kutotoa maneno hasi kuhusu Man United au amfukuze nafasi ya uwakilishi wake.

 

Nyota huyo amesema:-“Sifikiri kama klabu inatakiwa kujibu hilo, kwa nini ampe wakala muda wa kufanya hivyo? Paul Pogba ndiyo tatizo kwa sababu anamlipa (Raiola) kumwakilisha yeye (Pogba), na (Raiola) anamwakilisha vibaya na Pogba ni mtu mzuri.

 

“Kila mmoja nje ya klabu atajua (Pogba) ndiyo ana matatizo kumbe siyo, (Pogba) ana vitu viwili tu vya kufanya juu ya Raiola, amwambie anyamaze au amfukuze kazi,” amesema Scholes.

 

Kauli hiyo ya Scholes inakuja ikiwa ni siku mbili zimepita toka Mino Raiola atangaze kuwa Pogba hana furaha Man United na anataka kuondoka.  Hii inakuja baada ya kiungo huyo wa Ufaransa kutopata nafasi ya kucheza sana kama zamani. 


Nyota huyo inaelezwa kuwa anaweza kusepa ndani ya timu hiyo na kuibukia Klabu ya Juventus ambayo ilikuwa ni timu yake ya zamani.


SOMA NA HII  SIMBA KUSHUSHA WAMBA HAWA WANNE KUZIBA MAPENGO