Home Uncategorized MBAYA WA METACHA MNATA AKUBALI KUSAINI YANGA

MBAYA WA METACHA MNATA AKUBALI KUSAINI YANGA


BIGIRIMANA Blaise, mshambuliaji namba mbili ndani ya Namungo FC amesema kuwa anaweza kusaini Yanga iwapo utaratibu wa usajili utafuatwa.
Imekuwa ikielezwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoipasua kichwa Yanga ni pamoja na Blaise ambaye aliwatibulia Yanga walipokutana Machi 15 Uwanja wa Majaliwa kwa kusawazisha bao lao la mapema lililofungwa na Tariq Seif kwa kumtugua Metacha Mnata.
Blaise mwenye mabao 10 amesema kuwa amekuwa akiskia habari zake za kuwaniwa na Yanga hilo kwake ni jambo jema ila lazima utaratibu ufuatwe.

“Nina mkataba na Namungo kwa sasa ila unakaribia kuisha pale msimu utakapomalizika, ikiwa Yanga wanahitaji kupata saini yangu hakuna tatizo ni lazima utaratibu wa usajili ufuatwe mambo yakiwa sawa nitasaini bila tatizo,” amesema.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa wanawafuatilia wachezaji wa Namungo ili wasipate tabu dirisha la usajili likifunguliwa.
“Tupo na watu ambao wanajua mpira na tunawafuatilia wachezaji wote ndani ya ligi ikiwa ni pamoja na Namungo ila masuala ya usajili muda wake haujafika kwa sasa,” alisema.
SOMA NA HII  NOMA!! HUU NDIYO UBALAA WA MIPANGO YA YANGA MSIMU UJAO - VIDEO