Home Uncategorized REKODI ZA BIASHARA V PRISONS NI NOMA

REKODI ZA BIASHARA V PRISONS NI NOMA

LEO Desemba 22 Uwanja wa Karume, Mara kutakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Biashara United dhidi ya Tanzania Prisons huku rekodi zikinyesha kwamba Prisons haijawahi kupata ushindi mbele ya wapinzani wao.

Mchezo wa leo ni kwa ajili ya kukamilisha mzunguko wa kwanza ambapo, Biashara United inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza imecheza mechi 16 ipo nafasi ya tano kwenye msimamo na pointi zake ni 23.

Ndani ya uwanja tangu msimu wa 2018 mpaka leo msimu wa 2020/21 zimekutana uwanjani mara nne ambapo sare zimekusanywa tatu na ushindi ulikuwa mmoja uliokwenda kwa Biashara United.

Matokeo yao ilikuwa namna hii Novemba,07,2018 Biashara United Mara 0- 0 Tanzania Prisons, Uwanja wa Karume Memorial Stadium (Mara). April,6,2019 Tanzania Prisons 0- 0 Biashara United Mara, Uwanja wa Sokoine Stadium (Mbeya).

Oktoba,23,2019 Tanzania Prisons 0 -0 Biashara United Mara Uwanja wa Sokoine Stadium (Mbeya) na Machi ,4,2020 Biashara United Mara 1- 0 Tanzania Prisons, Uwanja wa Karume.


Ofisa Habari wa Biashara United, Idrisa Sechambo amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

SOMA NA HII  AZAM FC YATUMA UJUMBE HUU KWA MWADUI FC