Home Uncategorized RUVU SHOOTING YAITUPIA ‘DONGO’ KIMTINDO YANGA

RUVU SHOOTING YAITUPIA ‘DONGO’ KIMTINDO YANGA


 UONGOZI wa Ruvu Shooting mesema kuwa licha ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, jana Desemaba 6 bado wapinzani wake wanapata tabu kwenye umiliki wa mpira pamoja na kusaka ushindi jambo litakalowafanya wasifike mbali.


Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa mbinu na burudani ulichezwa Uwanja wa Mkapa ambapo mashabiki wa Yanga walijitokeza kushuhudia namna Ruvu inavyonyooshwa huku na wale wa Ruvu walijitokeza kuona namna pira gwaride litakavyopigwa kwa Mkapa.


Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa ameshangazwa na aina ya matokeo kwa kuwa walijipanga kushinda tangu awali ila kilichotokea ni sawa na hadhithi ya Yuda.


“Labda ninaweza kusema kwamba kwa namna ambavyo wapinzani wetu Yanga wamepata ushindi inaonekana kuna shida kidogo hasa ndani ya uwanja, licha ya kwamba wametushinda bado safari yao ina matatizo huko wanakokwenda.


“Ninafananisha na gari ambalo breki yake haifanyi kazi vizuri ukikanyanga kwa mguu sasa lazima utumie mkono ili kuweza kuisimamisha gari, kwa safari ya namna hii hakuna kitakachoweza kuwa salama labda sijui iweje.


“Kushindwa kwetu ninafananisha na habari ya Yuda kwa kweli sijui habari ya Yuda ipoje ila ukiitafuta na kujua namna hadithi yake ilivyo utajua tu,” amesema.


Yanga imejikita kileleni ikiwa imecheza mechi 14 bila kupoteza na ina pointi 34, Ruvu Shooting ipo nafasi ya nne na pointi zake ni 23.

SOMA NA HII  KOCHA TANZANITE AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO